Blatter:Sikujiuzulu kama rais wa FIFA

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Blatter:Sikujiuzulu kama rais wa FIFA

Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amekariri kuwa hakujiuzulu kama rais wa shirikisho hilo.

Kiongozi huyo mswissi mwenye mri wa miaka 79 alikuwa amedhaniwa kujiondoa madarakani juni tarehe 2 kufuatia kashfa kubwa ya ufisadi ulajirushwa na matumizi mabaya ya madaraka iliyokumba shirikisho lake lakini sasa anaonesha dalili za kubadili mtazamo huo.

Blatter ambaye ameiongoza FIFA kwa miaka 17 alikuwa ametangaza kuwa atajiondoa mbele ya kamati kuu ilikufanyike uchunguzi wa kina katika FIFA lakini sasa ameikumbusha jarida moja la uswisi BLICK kuwa yeye ndiye rais wa FIFA na kuwa aliweka hatima yake mikononi mwa kamati kuu ya shirikisho katika mkutano wa dharura.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hakuna mipango ya Blatter kuelekea Canada kwa Fainali ya kombe la Dunia la wanawake

Blatter anadhaniwa kuwa anafikiria kuwania tena uongozi wa shirikisho hilo.

Tuhuma za udhabirifu wa fedha ufisadi na ulaji rushwa ulianza katika ileile wiki ambayo Blatter alichaguliwa ikiendeshwa na Marekani.

Lakini punde baada ya uchaguzi utawala nchini Uswisi nao ukaanzisha uchunguzi sambamba wa ulaji rushwa na ufisadi dhidi ya maafisa wakuu katika shirikisho la soka duniani FIFA.

Blatter alistangaza kuwa anajiondoa uongozini ilikuruhusu uchunguzi ufanyike siku nne tu baada ya kuchaguliwa upya kwa hatamu ya uongozi wa FIFA.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ng'o Siondoki !

Kufuatia uchunguzi unaoendelea hakuna mipango na dalili zozote kuwa Blatter ama katibu mkuu wa FIFA

Jerome Valcke atakuwa mjini Ontario Canada katika fainali ya kombe la dunia kwa wanawake.

Kwa kawaida Blatter angekuwa huko ilikutoa zawadi ya kombe la dunia kwa timu itakayoibuka mshindi lakini hadi kufikia sasa hakuna mipango yoyote ya ziara hiyo.