Kenyatta: al Shaabab yaishiwa nguvu

Rais Kenyatta huku amevaa sare ya jeshi Haki miliki ya picha bbc

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amelaani siasa kali za baadhi ya Waislamu Afrika Mashariki.

Aliuambia mkutano wa kanda kuhusu usalama unaofanywa Nairobi kwamba kundi la Waislamu la al-Shabab limeishiwa nguvu na kwamba mashambulio yake ni ya kuinusuru tu al-Shabaab yenyewe, siyo kushinda.

Hapo Ijumaa, wapiganaji hao walishambulia kambi ya askari wa Umoja wa Afrika katikati mwa Somalia.

Wanajeshi wa kuweka amani kama 50 kutoka Burundi inaarifiwa waliuwawa.

Piya inaarifiwa kuwa wanajeshi wa Kenya walipambana na wapiganaji Ijumaa karibu na mji wa Dhobley, kusini mwa nchi.