Kuwait yaomboleza vifo vya watu 27

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kuwait yaomboleza vifo vya watu 27

Maombolezi yanaendelea nchini kuwait kuwakumbuka watu 27 waliouawa kwenye shambulizi la kujitoa mhanga kwenye msikiti wa kishia.

Wakati huo huo msemaji wa kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini kuwait anasema kuwa usalama umedumishwa katika vituo vyote vya mafuta kote nchuni humo baada ya shambulizi ambalo Islamic State wanasema kuwa walihusika.

Islamic State huwaita waislamu wa madhehebu wa shia kuwa wazushi na hivi majuzi walishambulia misikiti yao miwili katika nchi jirani ya Saudi Arabia.