Ulaya yakubali kuipa Ugiriki mkopo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ulaya yakubali kuipa Ugiriki mkopo

Benki kuu ya ulaya ECB imeafikiana kuendelea kuzifadhili benki za Ugiriki na kuwa

haitozidisha kiwango cha mkopo wa dharura inayoyapa mabenki ya Ugiriki kuambatana na mapatano yaliyopendekezwa ijumaa iliyopita..

Uamuzi huo unafuatia mazungumzo kuvunjika.

Mazungumzo baina ya Ugiriki na nchi zinazotumia sarafu ya euro, kuhusu mpango wa kurekibisha uchumi wa Ugiriki, uliopendekezwa na wakopeshaji.

Ugiriki haitaki kuridhia mpango huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maelfu ya wagiriki wamekuwa wakichukua pesa zao kutoka kwenye akaunti za benki

ECB imesema kuwa iko tayari kufanya mabadiliko yeyote kuambatana na kanuni za mfuko wa dharura kwa ushirikiano wa karibu na benki kuu ya Ugiriki.

Kwa mujibu wa mhariri wa BBC wa maswala ya Uchumi na Biashara Robert Peston Benki hiyo ya Ulaya imekataa kuingozea pesa zaidi kwa mkopo.

Kauli hiyo inamaanisha kuwa mabenki ya Ugiriki yatakuwa na wakati mgumu kuhimili matakwa ya wateja wake na uchumi kwa jumla.

Aidha uamuzi wa ECB, huo utamaanisha kuwa mabenki ya Ugiriki, huenda yakawa hayana pesa taslim za kutosha, kuruhusu wateja kutoa pesa, na pengine mabenki hayatoweza kufunguliwa kesho.

Mabenki ya Ugiriki yanategemea mfuko huo wa dharura wa benki ya ulaya kwa mahitaji ya kuendesha biashara yao ya siku hadi siku.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bwana Tsipras kwa upande wake amewataka wagiriki kupiga kura ya hapana kwenye kura ya maoni

Mawaziri wa fedha wa nchi za ulaya wanasema kuwa Ugiriki itahitaji kudhibiti pesa zinazotolewa kwenye mabenki.

Kauli hiyo imewadia baada ya mkutano wa mawaziri wa fedha na uchumi kutoka mataifa yanayotumia sarafu ya Euro.

Aidha mkutano huo umefanyika baada ya bunge la Ugiriki kuunga mkono mpango wa waziri mkuu wa nchi hiyo Alexis Tsipras wa kuandaa kura ya maoni kuhusu pendezo la hivi punde zaidi la kuipa mkopo ugiriki.

Benki kuu ya ulaya itahitajika kuamua ikiwa mikopo itatolewa kwa Ugiriki ili kuzuia kuanguka kwa mabenki yake.

Bwana Tsipras kwa upande wake amewataka wagiriki kupiga kura ya hapana kwenye kura ya maoni ambayo itafanyika tarehe 5 mwezi Julai.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Amesema kuwa kura ya hapana itaipa Ugiriki uwezo wa kufanya majadiliano.

Amewalamu wakopeshaji wa nchi hiyo wakiwemo muungano wa ulaya, benki kuu ya Ulaya na shirika la fedha duniani IMF kwa kuihangaisha Ugiriki.

Amesema kuwa kura ya hapana itaipa Ugiriki uwezo wa kufanya majadiliano.

Maelfu ya wagiriki wamekuwa wakipiga foleni na kuchukua mabilioni ya Euro kutoka kwenye akaunti zao za benki wakihofia kuwekewa vikwazo.

Mawaziri wa fedha wa nchi za euro, wame-pe-nde-keza kuwa Ugiriki inafaa kutangaza kesho kuwa siku ya mpumziko, ili kudhibiti mtafaruku wa kifedha ukitokea