Aliyejilipua Kuwaiti ni raia wa Saudi

Haki miliki ya picha none
Image caption Aliyejilipua Kuwaiti ni raia wa Saudi

Vyombo vya habari nchini Kuwaiti zinasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliyejilipua ndani ya msikiti nchini humo Ijumaa na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 25 ni raia wa Saudi Arabia.

Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya usalama wa ndani nchini Kuwait mshambuliaji huyo anatambuliwa kuwa ni Fahd Suliman Abdul-Muhsen al-Qabaa.

Yamkini taarifa hiyo inasema kuwa Fahd alikuwa ametua katika uwanja wa kimataifa wa ndege ulioko Kuwaiti saa chache kabla yake kutekeleza shambulizi hilo la kwanza kutokea nchini humo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyejilipua Kuwaiti ni raia wa Saudi Arabia

Takriban watu 27 wamethibitishwa kufariki katika shambulizi hilo ambalo serikali ya Kuwaiti inasema kuwa inalenga kuchochea uhasama wa kidini baina ya Wasuni na Washia wa Kuwaiti.

Kulingana na maafisa wa uhamiaji, Fahd alikuwa nchini humo kinyume cha sheria.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Takriban watu 27 wamethibitishwa kufariki katika shambulizi hilo

Kundi la wapiganaji la Islamic State limedai kuwa Fahd Suliman Abdul-Muhsen al-Qabaa ni mmoja wao.

Kundi hilo linawakashifu waislmu washia kuwa wanakufuru na kukiuka maadili haswa na mafundisho ya mtume Muhammad.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Fahd alikuwa ametua katika uwanja wa kimataifa wa ndege ulioko Kuwaiti saa chache kabla yake kutekeleza shambulizi hilo

Mwezi uliopita tawi la Saudi Arabia la Islamic State lilitekeleza mashambulizi katika misikiti ya washia nchini humo.

Mashambulizi haya haswa kwa mataifa yanayochangia jeshi la muungano linalopigana na Wahouthi nchini Yemen na Islamic State nchini Syria na Iraq yamefikisha ujumbe wa ugaidi nyumbani kwa mataifa ya kanda hiyo ya ghuba kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa maswala ya Mashariki ya kati na ghuba Sebastian Usher.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Takriban watu 200 wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo

Takriban watu 200 wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo lililoibua hofu miongoni mwa waislamu washia nchini humo.

Kuwait inaidadi kubwa ya washia katika kanda hiyo.