Maelfu ya watalii waondoka Tunisia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya watalii waondoka Tunisia

Maelfu ya watalii wameondoka nchini Tunisia kufuatia shambulizi la siku ya Ijumaa kwenye eneo moja la ufuo wa bahari ambapo watu 38 waliuawa wengi wakiwa kutoka ulaya.

Afisa anayehusika na masuala ya utalii katika eneo la Sousse amesema kuwa wageni zaidi ya 3000 wameondoka eneo hilo tangu mauaji hayo yafanyike.

Serikali mjini Tunis inasema kuwa usalama umedumishwa lakini makampuni ya watalii tayari yameanza kufuta safari.

Serikali ya uingerezea imesema imethibitisha kuwa takriban raia 15 wa nchi hiyo ni miongoni mwa wale waliouawa.

Kundi la Islamic State linasema kuwa ndilo lililohusika kwenye shambulizi hilo.