Wanajeshi 11 wauawa Afghanistan

Image caption Taleban

Wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan wamedaiwa kuwaua wanajeshi 11 katika jimbo la Herat magharibi mwa taifa hilo.

Msemaji wa serikali katika eneo hilo, amesema kwamba walinda usalama hao walikuwa ndani ya magari ya wazi pamoja na malori pale msafara wao uliposhambuliwa na wanamgambo wa Taliban.

Wanajeshi wanne walijeruhiwa katika kisa hicho.

Kufikia sasa kundi hilo bado halijakiri kuhusika na kabiliano hilo.

Wapiganaji hao wa Taleban wameimarisha mashambulizi yao dhidi ya wanajeshi tangu wazindue mashambulizi yao mwezi Aprili.

Jeshi la Afghanistan limekumbwa na maafa chungu nzima mwaka huu kwa kuwa linapigana bila usaidizi wa vikosi vya NATO ambavyo vilikamilisha oparesheni zao miezi sita iliopita.