Kiongozi wa mashtaka ajeruhiwa Misri

Haki miliki ya picha
Image caption Hisham Barakat

Maafisa wa usalama nchini Misri wanasema kuwa shambulio katika mji mkuu, Cairo, limemjeruhi kiongozi wa mashtaka, Hisham Barakat.

Wamesema shambulizo hilo lililenga msafara wa Bwana Barakat katika wilaya ya Heliopolis nje ya chuo cha kijeshi.

Shambulizi hilo linafanyika baaada ya kundi linaloshirikishwa na Islamic state huko Misri kuitisha mashambulizi baada ya hukumu ya mahakama kutolewa kuwa wapiganaji sita wanyongwe.

Bwana Barakat amekuwa akipendekeza mamia ya wapiganaji hao kufunguliwa mashtaka tangu kupinduliwa kwa rais aliyependuliwa , Mohamed Morsi, mwaka 2013.