Benki za Ugiriki kufungwa kwa wiki moja

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wapigani foleni ili kutoa fedha katika mashine za ATM kufuatia kufungwa kwa benki nchini Ugiriki

Serikali ya Ugiriki imethibitisha kuwa benki zake zitafungwa kwa kipindi cha juma moja kufuatia uamuzi wa Benki kuu barani Ulaya wa kutoendelea kutoa fedha za kukabiliana na dharura.

Utoaji wa fedha katika mashine za ATM utadhibitiwa huku watu wakiruhusiwa kutoa Yuro sitini kwa siku,hatahivyo masharti hayo hayatawaathiri raia walio na kadi za benki za kigeni.

Katika hotuba iliopeperushwa na runinga za taifa hilo Waziri mkuu nchini Ugiriki Alexis Tsipras ameomba utulivu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Benki

Mwandishi wa BBC mjini Athens amesema kuwa hakuna ishara za wasiwasi huku raia wakionekana kuelekea makazini kama kawaida.

Hatua hiyo ya benki kuu ya Ulaya inafuatia kuanguka kwa mazungumzo katika ya Ugiriki na mataifa ya Ulaya kuhusu makubaliano yanayokwisha siku ya jumanne ya kulikwamua taifa hilo kutoka kwa madeni yake,siku ambayo taifa hilo linafaa kulipa Hazina ya fedha duniani dola bilioni 1.6.