Indonesia: 141 waliaga dunia

Image caption Indonesia inasema kuwa idadi ya watu waliofariki huko Medan katika ajali ya ndege ya kijeshi imepanda na kufikia watu 141.

Indonesia inasema kuwa idadi ya watu waliofariki huko Medan katika ajali ya ndege ya kijeshi imepanda na kufikia watu 141.

Kulingana na taarifa ya jeshi la wanahewa nchini humo hakuna yeyote aliyenusurika kifo miongoni mwa watu 122 waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya mizigo chapa Hercules C-130.

Jeshi limesema kuwa limeanzisha uchunguzi kubaini haswa ni nani waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya kijeshi baada ya uvumi kuenea kuwa ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria waliokuwa wamelipa nauli.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 113 ilipoanguka.

Taarifa kutoka kwa jeshi imesema kuwa wale wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo ambao sio jamaa ya wanajeshi hawatafidiwa.

Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 113 ilipoanguka.

Kuna ushahidi kuwa takriban watu 19 waliokuwa ardhini waliuawa.

Afisa mkuu wa jeshi la wanahewa Air Marshall Agus Supriatna amesema kuwa hakuna manusura waliopatikana hai.

Image caption Baadhi ya jamaa waliofiwa katika ajali hiyo ya ndege

Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ilizoangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.

Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.

Afisa wa polisi Agustinus Tarigan amewaambia waandishi wa habari katika Hospitali ya Medan kuwa miili 141 imepokewa.

Ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Medan ikielekea kisiwa cha Tanjung Pinang,kilichoko Sumatra inasemekana kuwa ilikuwa ikitoa moshi na moto kabla ya kuangukia majengo na makaazi watu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shughuli ya uokoaji inaendelea

Ndege hiyo ilikuwa ikigeuka kurejea katika uwanja wa ndege ilipoanguka.

Rais wa Indonesia Joko Widodo ametuma risala za rambirambi kupitia mtandao wake wa twitter akiwatakia wahasiriwa ''Subira na nguvu''wakati huu wa msiba.

Ameliagiza jeshi lifanye mabadiliko ya kina katika usafiri wa wanajeshi ilikuzuia maafa kama hayo yaliyotokea.