Caitlyn Jenner ni mwanamke mshawishi

Image caption Caytlin Jenner

Mtu aliyejibadilisha maumbile na kuwa mwanamke Caitlyn Jenner ameorodheshwa miongoni mwa wanawake 10 mashuhuri wenye ushawishi mkubwa pamoja na Angelina Jolie,Singer Sia na Anna Wintour.

Orodha hiyo iliyoongozwa na waziri wa kwanza wa Uskochi Nicola Sturgeon inawatambua wanawake ambao wamekuwa wakiathiri uma pakubwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Angelina Jolie

Nyota wa kipindi cha Keeping up with the Kardashians Jenner aliyejulikana kama Bruce ameorodheshwa katika nafasi ya saba.

Alibadilisha maumbile yake na kujiita Caitlyn katika jarida la Vanity Fair mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nicola Sturgeon

Mwanariadha huyo wa zamani ambaye wanawe ni pamoja na mwana wa kambo Kim Kardashian na Kendall Jenner ametunukiwa heshima ya kuonyesha maumbile yake mapya kwa uma.