Gari laingia katika paa ya nyumba

Image caption Gari

Mapema leo gari liligonga na kuingia ndani ya nyumba moja nchini Afrika Kusini kupitia paa la nyumba hiyo kulingana na huduma ya dharura ya ER24 nchini humo.

Image caption Gari

Dereva wa gari hilo amesema kuwa alipokuwa akiliendesha gari hilo alikutana na tuta moja barabarani lililosababisha gari hilo kuruka na kuanguka katika paa la nyumba hiyo.

Image caption Gari

Bado haijulikani ni vipi tuta hilo lilisababisha ajali hiyo.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa na dereva wa gari hilo hakupata jeraha lolote.