Msumbiji yakubali mapenzi ya jinsia moja

Wapenzi wa Jinsia moja Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nchi chache Afrika zimekubali mapenzi ya jinsia moja

Msumbiji imehalalisha mapenzi ya jinsia moja,na kuwa moja wapo wa nchi chache Afrika zinazohalalisha mapenzi ya jinsia moja.

Sheria hiyo iliyowekwa na wakoloni wa nchi hiyo Ureno iliondolewa na bunge la nchi.Watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja,wametaja hatua hiyo kama ushindi mkubwa.

Hata hivyo nchi nyingi za Afrika zimeweka sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.Nigeria ilipiga marufuku na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.Uganda nayo imeapa kurejesha sheria kali kuharamisha mapenzi ya jinsia moja.

Sheria ya awali ilitupiliwa nje na mahakama ya kikatiba.

Msumbiji sasa anajiunga na mataifa mengine ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ivory Coast na Afrika Kusini ambapo siyo hatia kuwa mpenzi wa jinsia moja.