Kura ya maoni Ugiriki kutoa suluhu?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkuu wa Shirika la fedha duniani, Christine Lagarde

Mkuu wa Shirika la fedha duniani, IMF, Christine Lagarde amesema ana matumaini kuwa matokeo ya kura ya maoni ya Ugiriki kuhusu hali ya uchumi wa nchi hiyo yataweka wazi na uhakika kuhusu hali ya nchi hiyo

Bi Lagarde amesisitiza kuwa mabadiliko ya kiuchumi ya Ugiriki yapewe kipaumbele kabla ya wakopeshaji wa kimataifa hawajatoa msaada mpya wa kunusuru uchumi wa nchi hiyo.

Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras,amewaambia watu wake kukataa masharti ya mkopo ambayo yanalazimu hatua zaidi za kubana matumizi.

Lakini Benki kuu ya Ulaya imesema itaendelea kutoa fedha za dharura kwa Benki za nchi hiyo.