Uhuru Kenyatta ndio rais bora Afrika

Image caption Uhuru Kenyatta ndiye rais bora barani Afrika

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amechaguliwa na muungano wa wanafunzi wa Vyuo vikuu barani Afrika AASU kama rais bora barani Afrika mwaka huu.

Muungano huo unasema kuwa maelfu ya wanafunzi kutoka kote barani walishiriki katika kura hiyo.

Bwana Kenyatta alichaguliwa kwa uwezo wake wa kujenga makubaliano kitaifa na kimataifa,juhudi zake za kubadilisha sera na kutoa ufumbuzi katika maswala yanayowaathiri wakenya.

Rais wa Rwanda Paul Kagame alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita.