AMISOM:Hatutaondoka Somalia

Image caption Wanajeshi wa Amisom nchini Somalia

Wanajeshi wa umoja wa Afrika nchini Somalia Amisom hawataondoka katika miji yoyote ya kusini mwa Somalia kinyume na ripoti za vyombo vya habari,kwa mujibu wa Amisom

Kumekuwa na ripoti kwamba wanajeshi hao wamekuwa wakiondoka katika miji mitano ya Somalia,lakini mwakilishi wa Umoja huo nchini Somalia balozi Maman Sidikou amesema kuwa huo ni uvumi unaolenga kuzua hofu.

Ameongezea kuwa vikosi vya AU vinapangwa kuendeleza vita dhidi ya kundi la La Alshabaab.