Masoko ya fedha yapata hasara Uchina

Soko la hisa China Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Soko kuu la Shanghai hisa zimesuka kwa asili mia sita

Bei ya hisa nchini China imeendelea kushuka licha ya hatua ya serikali kuyachepua masoko ya fedha katika siku za karibuni.

Soko kuu la hisa la Shanghai lilifunga biashara yake kwa bei iliyopungua kwa asili mia sita.

Kampuni za serikali zimekua zikinunua hisa ili kuimarisha bei.Serikali ya China imesema inachunguza madai ya kuchezea bei ya hisa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wawekezaji wamekua na wasi wasi kuhusu hali katika masoko ya fedha

Kwa mwaka mmoja bei ya hisa China iliimarika mara dufu.Hata hivyo hali iligeuka mwezi uliopita ambapo bei ilianza kushuka.

Kuna wasi wasi kuhusu imani ya wakewezaji milioni 90 wa Ki-China ambao wadadisi wanasema tayari wameanza kuhofia hali katika masoko ya fedha nchini humo.