Tohara ya milimani Afrika Kusini

Vijana wanaotahirishwa Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vijana wanaotahiriwa

Mrengo wa vijana katika chama tawala Afrika Kusini{ANC Youth League} umesema unapanga kufanya sherehe ya tohara ya kitamaduni kwenye milima maalum.

Shirika la Turathi la Umoja wa Mataifa{UNESCO} limetangaza eneo hilo la "Table Mountains" kuwa turathi kwa sababu kuna mimea ya kipekee. Kuna aina elfu tano ya mimea kwenye milima hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Vijana wa ANC wanataka kufanya sherehe ya tohara milimani

Taarifa ya vijana hao wa ANC jimbo la Western Cape imesema hakuna arthi ya kufanyiwa tohara ya utamaduni. Haijabainika ikiwa watapata idhini kuendesha shughuli hiyo.