Mlipuko msikitini wawaua watu 25 Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msikiti walipuliwa nchini Syria

Wanaharakati nchini Syria wanasema kuwa mlipuko kwenye msikiti mmoja katika mkoa ulio kaskazini magharibi wa Idlib umewaua takriban wanachama 25 wa kundi lenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda la Al Nusra Front.

Shirika la haki za binadamu lenye makao yeke nchini Uingereza linasema kuwa mlipuko huo kwenye mji wa Ariha ulitokea wakati wanachama wa kundi hilo walipokutana kupata chakula.

Haijabainika ni nani aliendesha shambulizi hilo.

Mapema ndege za kivita za Syria zilishambulia waasi karibu na mji wa Aleppo kuzima jaribio ya kutaka kuuteka mji huo.

Utawala nchini Syria unasema kuwa takriban wanamgambo 100 waliuawa.