Baba Mtakatifu Francis awasili Ecuador

Image caption Baba Mtakatifu Francis, akisalimia jamii za Ecuador.

Baba mtakatifu Francis amwasilini nchini Ecuador akiweka kituo cha kwanza katika ziara yake itakayodumu kwa siku saba,akizuru upande wa Amerika Kusini, ambao ni makabwela watupu.

Akiwa ndio amewasili nchini humo,amesema kwamba kila mmoja katika jamii anapaswa kufaidika kutokana na shughuli za kimaendeleo duniani.

Maelfu ya watu walikuwa wakisubiri kumlaki baba mtakatifu katika mitaa ya nchi hiyo na hasa katika mji mkuu, Quito.

Baba mtakatifu Francis, ambaye ni mzaliwa wa Argentina, atafanya ziara pia katika nchi za Bolivia na Paraguay.

Awali baba mtakatifu huyu alinukuliwa akiielezea Amerika Kusini japokuwa ni masikini! Jamii zake zinapaswa kuwa na usawa kama zilivyo nchini nyingi ulimwenguni.