IS washambuliwa vikali mjini Raqa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption IS washambuliwa vikali mjini Raqa

Muungano unaongozwa na Marekani unasema kuwa umefanya mashambulizi makubwa ya angani dhidi ya wanamgambo wa islamic state katika ngome yao kuu ambao ni mji wa Raqa.

Msemaji wa Mareknai aliyataja mashambulizi hayo kuwa moja ya makubwa zaidi kuwai kuendeshwa nchini Syria hadi leo akisema kuwa lengo kuu lilikuwa ni kuwazuia IS kuondoa wapiganaji wake kutoka mji huo.

Shirika moja la waangalizi lilisema kuwa ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani ilishambulia shule mjini Raqa ambapo raia watatu waliuawa akiwemo mtoto na mwanamgambo wa Islamic State.