Ugiriki yazidi kuwekewa vikwazo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msururu wa raia wa Ugiriki katika benki nchini humo

Benki kuu ya jumuiya ya Ulaya imeongeza mbinyo wa mfumo wa kifedha kwa Ugiriki ,siku moja baada ya taifa hilo kupiga kura ya hapana dhidi ya masharti ya kimataifa kuhusiana na madeni yake.

Benki hiyo imekataa kuongezea muda kwa benki za Ugiriki kulipa madeni yake na kutaka kuweka mazingira salama ya deni la sasa ambalo ni euro 89 bilioni.

Hata hivyo benki zinatakiwa kuendelea kufungwa hadi siku ya Jumatano ambapo pia udhibiti wa utoaji fedha utaendelea.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya uchumi anasema kuwa msimamo huo wa ECB utasababisha mfumo wa kibenki nchini humo kukwama.