Hungary

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Polisi wa Hungary wakikagua mipaka yao

Bunge la Hungary limepitisha sheria ambayo itaipa nguvu serikali yake kufunga mipaka yake yote kwa ajili ya wakimbizi wote.Bunge hilo limekubali ujenzi wa uzio wenye urefu wa mita nne kwenda juu katika mpaka wa Serbia ili kuzuia kumiminika kwa watu katika ukanda huo. Mamia ya watu huingia kinyume na sheria kila siku.Msemaji wa serikali amedhibitisha kuwa mamlaka ya eneo hilo imeichukulia Serbia,Macedona,Bulgaria na Ugiriki kuwa ni nchi salama kwa kumaanisha kuwa maombi ya hifadhi katika nchi karibu zote za nchi hizo imefungwa. Hata hivyo kabla ya kura ,wakala wa shirika la umoja wa kimataifa linalosimamia masuala ya wakimbizi limesema kuwa maamuzi hayo yatawaathiri maelfu ya wa watu ambao wanatafuta hifadhi salama.