UN na miaka 20 ya mauaji ya Bosnia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mama akiomboleza kwenye kaburi la nduguye

Mipango ya upigiaji kura wa rasimu ya kura ya maoni ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka ishirini tangu kutokea kwa mauaji ya halaiki katika mji wa Srebrenica nchini Bosnia,imesitishwa baada ya Urusi kutishia kupiga kura ya veto.

Azimio la rasimu hiyo lililoandaliwa na Uingereza na kisha kutumia neno mauaji ya kimbari neno ambalo limekataliwa na nchi za Urusi na Serbia.

Hoja wanayoitoa ni kwamba kuna mkanganyiko wa mambo juu ya juhudi za maridhiano nchini Bosnia.watu elfu elfu nane wanaume na wavulana waliuawa na wanajeshi ya Bosnia ambayo yaliuvamia mji uliokuwa chini ya wa himaya ya Umoja wa mataifa.

Urusi tayari imekwisha sambaza rasimu mbadala ambayo ina mambo yote bila kutaja mauaji ya kimbari.