Marekani kuimarisha uhusiano na Vietnam

Image caption Rais Barack Obama akiwa na jamii ya wa Vietnam Ikulu ya Marekani.

Rais Barack Obama amefanya mazungumzo na kiongozi wa chama cha jamii ya wavietnam,Ikulu ya Marekani mapema wiki hii,mkutano ambao ni wa kwanza tangu nchi hizo mbili kurejesha uhusiano baada ya miaka ishirini iliyopita.

Rais Brack Obama amesema kwamba pamoja na kutofautiana kwa falsafa za kisiasa,nchi mbili hizo zilihitaji ushirikiano wa dhati,ikumbukwe kwamba mwezi huu imetimia miaka arobaini tangu kwisha kwa vita vya Vietnam.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba Rais Obama anasaka kuweka historia ya serikali yake kutoka katika uhusiano tete na Vietnam na kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimkakati dhidi China.