New Zealand kudhibiti mitandao

Haki miliki ya picha Getty
Image caption New Zealand kudhibiti mitandao

New Zealand inautangaza udhalimu unaoendeshwa kupitia kwa mitandao kuwa uhalifu.

Mswada wa mawasiliano ya digitali unaotajwa kuwa wenye athari uliidhinishwa na bunge wiki iliyopita na unatarajiwa kuanza kutekelezwa siku ya Jumatatu.

Hii inamaanisha kuwa watu watapigwa faini au kufungwa jela kwa kutumia lugha ya vitisho au ya kakandamiza kupitia mitandaoni.

Pia litabuniwa shirika ambalo litashirikiana na mitandao kama Facebook, Google na Twitter kuondoa lugha kama hizo.

Wakosoaji wanasema kuwa sheria hiyo itakandamiza uhuru wa kusema.