Dilma Rousseff asema kamwe hatishiki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Rousseff amewataka wapinzani wake watafute ushahidi dhidi yake

Huku kukiongezeka tuhuma kuhusu mustakabali wa serikali yake, rais Dilma Rousseff ameliambia gazeti la Folha de Sao Paulo kwamba 'hatoanguka' n kwamba hakuna msingi wa yeye kuachishwa kazi na bunge.

Ikiwa ni miezi saba baada ya kuingia katika muhula wake wa pili wa uongozi , serikali yake inatikiswa na kashfa ya rushwa katika kampuni kubwa ya mafuta nchini Petrobras.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji dhidi ya serikali ya Rousseff

Tuhuma za hivi karibuni zinadai kwamba kampeni yake ya kuwania urais ilifadhiliwa kwa pesa haramu kutoka kampuni hiyo.

Umaarufu wa Rousseff umedidimia kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha asilimia 9.

Siku ya Jumanne ameliambia gazeti hilo la Folha de Sao Paulo kwamba hatishiki.

Amekana kufanya makosa yoyote na amesema hivi ni vita vya kisiasa na amewataka wapinzani ake watafute ushahidi dhidi yake.