Tunisia kujenga ukuta kati yake na Libya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Takriban watu 38 waliuawa katika shambulio la Sousse

Waziri mkuu wa Tunisia Habib Essid ametangaza mpango wa serikali yake wa kukabiliana na ugaidi kufuatia shambulio dhidi ya watalii huko Sousse lililotekelezwa na mwanamgambo aliyeshawishika na kundi la IS mwezi uliopita.

Serikali ya Tunisia inajitahidi kutoa hakikisho kwa raia wake na ulimwengu kwa jumla kwamba inaweza kukakabiliana na tishio kutoka kwa wanamgambo wanaoshawishiwa na kundi la Islamic State.

Sekt yake muhimu ya utalii inakadiriwa kupoteza dola nusu bilioni mwaka huu baada ya shambulio hilo la Sousse na jingine lililotokea awali katika jumba kuu la ukumbusho nchini humo.

Mwanamume huyo aliyetekeleza mauaji ya Sousse anaaminika kupokea mafunzo huko Libya ambako ghasia zilizojiri nchini humo ziliruhusu kushamiri kwa wanamgambo wenye itikadi kali za dini ya kiislamu.

Waziri mkuu anasema ukuta huo utakamilika kufikia mwisho wa mwaka huu, na utajengwa kilomita 160 kati ya mpaka wa kuvuka pwani na mwingine kuingia Dehiba.