Mbinu ya kuwakumbuka mashujaa wanawake

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Zaidi ya wanawake 100 wamo katika programu hii

Waanzilishi programmu hiyo iitwayo ‘women on the map’ wana wasiwasi kuwa wanawake waliofanya maswala yanayohitaji kuangaziwa hawatajiki kama vile wanaume.

Programu hii itakuwa sehemu ya progamu nyingine ya kampuni ya google, ya ‘field trip app’ inayo onyesha mahala mashuhuri unapotembelea eneo flani.

Wateja watahitajika kuwezesha programu hiyo kwenye simu zao ili waweze kupata arafa wakiwa katika maeneo ambapo mwanamke amefanya kitu cha umaarufu flani na basi kupata ujumbe wa yale aliyofanya na pia kumhusu yeye binafsi.

Imewalenga wanawake kati ya miaka 13 na 22 na itawezeshwa ulimwengu nzima.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Imewalenga wanawake kati ya miaka 13 na 22

Kwa mfano kama unatamembelea jiji la Santiago nchini Chile, programu itakupa arafa ya kundi la Arpilleristas ambalo hushona nguo ambazo kwa kawaida kuwekwa ukutani na huwa za rangi tofauti.

Zaidi ya wanawake 100 wamo katika programu hii wenye kufanya vitu vya kipekee lakini inatarajiwa wanawake wengine watajiunga nayo.

Kundi la Spark lenye mradi huu lina wanawake thelathini walio chini ya miaka 23.

Kundi hili linataka watu wawatumie wasifu wa maneno 150-300 wa wanawake walio wagusa moyo.

Mwanamke huyo huenda akawa wa eneo anakotoka mtu au ni mwanamke wa jadi.