Ulaghai wadaiwa katika soko la hisa Uchina

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ulaghai wadaiwa kushamiri katika soko la hisa la Uchina

Huku bei ya hisa zikiimarika nchini Uchina, wasimamizi wa sekta za uchumi nchini humo wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kile shirika la habari limetaja kuwa ulaghai katika soko la hisa.

Ripoti zinasema kuwa wawekezaji wamekuwa wakiuza hisa kwa mpango ili kushusha bei.

Uamuzi huu ni wa tatu wa serikali ya nchi hiyo wa kunusuru bei za hisa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, ambapo bei za hisa zilipoteza thamani ya zaidi ya asilimia ishirini na tano.

Mwandishi wa BBC anasema chama tawala cha kikomunisti kimeanikwa wazi huku baadhi ya maamuzi yake ya kuimarisha bei yakifanya mambo hata kuwa mbaya zaidi.