Rebecca Garang: Viongozi wamefeli S Kusini

Haki miliki ya picha
Image caption Rebecca

Mama wa taifa la Sudan Kusini Rebecca Garang amesema kuwa viongozi wa taifa hilo akiwemo yeye mwenyewe wamewafeli raia.

Juhudu za kuafikia mkataba ili kumaliza mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea zimefeli.

Amesema kuwa licha ya mgogoro uliopo, uhuru uliopatikana ulistahili kwa kuwa utavisaidia vizazi vijavyo.

Marekani imesema kuwa pande zote mbili katika mgogoro huo zina hatia.

Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani Susan Rice amewataka viongozi wa pande zote kuwacha tofauti zao huku akionya kuwa wale watakaoendelea kulitokomeza taifa la Sudan Kusini wataadhibiwa.