Wakimbizi wa Syria wamezidi milioni 4

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ulaya inaombwa kuchukua jukumu la pamoja kukabiliana na hali

Idadi kubwa ya wakimbizi wa Syria wamo katika nchi jirani, ambazo rasilmali zao na muundo wa kijamii unalemazwa.

Mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi, Antonio Guterres, ameimabia BBC kwamba mataifa yote ya Ulaya ni lazima yaelewe kwamba hii ni hali ambayo nchi zote haziwezi kuiepuka. Aliyasema hayo alipokuwa akitangaza wimbijipya la wakimbizi wa Syria wanaokwepa mzozo lilisababisha idadi ya wakimbizi hao kuongezeka na kuzidi milioni nne.

Huku zaidi ya watu elfu sabiini wakiwasili Ugiriki na wengine wengi wakitarajiwa kuingia wakati wa msimu wa joto, Guterres amesema Ulaya inahitaji kuchukua jukumu la pamoja kwa anachokitaja kuwa mzozo usiomalizika na usiokuwana matuamini mwishowe.