Afghanistan yazungumza rasmi na Taliban

Image caption Mazungumzo ya amani na Taliban Pakistan

Ujumbe wa kwanza rasmi wa serikali ya Afghanistan kufanya mazungumzo na kundi la Taliban limerudi katika mji mkuu Kabul, awamu nyengine ya mazungumzo huenda ikafanyika China.

Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa kuhusu mazungumzo hayo, serikali ya Afghanistan inasema ndio mara ya kwanza mazungumzo ya ana kwa ana yanafanyika na wapiganaji wa Taliban.

Kiongozi wa ujumbe wa serikali - naibu waziri wa mamabo ya nje Hekmat Karzai, amesema tofuati muhimu kati ya mazungumzo haya na ya awali ni kuwa mara hiii yalikuwa rasmi kwa pande zote mbili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mojawapo ya wapiganaji wa Taliban walioshiriki mazungumzo hayo

Ameshawishika kwamba amekutana na watu walio na uwezo wa kujadili kwa niaba ya uongozi wa Taliban.

Na muhimu zaidi walionekana kuakilisha mtandao unaojulikana kama Haqqani, kundi la wanamgambo lililopo Pakistan, linaloshirikiana na Taliban.

Marekani na China zilikuwa na mwaangalizi rasmi katika mazungumzo hayo, na mmojawapo ya wajumbe wa serikali ya Afghanistan amesema mazungumzo ya siku zijazo baada ya sikukuu ya Eid huenda yakafanyika China.

Licha ya matumaini haya ya serikali ya Afghanistan, kuna hisia tofuati zinazotoka kwa Taliban kuhusu iwapo kwa upande wao ulikuwa ujumbe rasmi unaowakilisha kundi hilo zima.