Udukuzi wampeleka jela raia wa Israel

Image caption Madonna

Mwanaume mmoja nchini Israel,amehukumiwa kifungo cha miezi kumi na nne huko Tel Aviv kwa kudakua komputa ya waimbaji akiwemo Madonna.

Madona ilimbidi azindue nyimbo zake sita kwa haraka kutoka kwenye albamu yake mpya baada ya nyimbo hizo kuvuja kwenye mitandao mwezi wa desemba.

Adi Lederman mwenye umri wa miaka thelathini na tisa alifungwa mwezi january mara baada ya uchunguzi uliosaidiwa kufanywa na shirika la kijasusi la FBI.

Lederman amekubali tuhuma hizo za kukiukwa kwa faragha za mtu binafsi na mali zake. Madona ilimbidi azindue nyimbo zake sita kwa haraka kutoka kwenye albamu yake mpya baada ya nyimbo hizo kuvuja kwenye mitandao mwezi wa desemba.