Waandishi Ethiopia waachiliwa huru

Image caption Nembo ya wanablogu hao wa Zone 9 Ethiopia

Waandishi hao watatu ni sehemu ya wanablogu 9 na waandishi habari ambao kwa pamoja wanajulikana kama Zone 9 bloggers.

Miongoni mwa walioachiliwa ni waandishi Tesfalem Waldyes na Asmamaw Hailegeorgis na aliyekuwa mhadhiri katika chuo kikuu na mwanablogu Zelalem Kiberet.

Wote walikamatwa April 2014. Kuzuiwa kwao kumezusha shutuma kali dhidi ya serikali ya Ethiopia inayoshutumiwa kwa kundamiza uhuru wa vyombo vya habari na upinzani nchini.

Wakili wao anasema anafurahi kwamba kuteswa kwao kumemaliza lakini ataendelea kushinikiza kuachiliwa kwa wengine sita wanaoendelea kuzuiwa.