Bango lamuua mwanafunzi Afrika Kusini

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Maafisa wanachunguza kisa hicho kwa makini.

Walioshuhudia mkasa huo wanasema mvulana huyo alikuwa anachungulia nje ya dirisha wakati basi alimokuwa lilipita katika barabara nyembamba mjini.

Polisi wameliziba eneo hilo na kuufinika mwili na mablanketi kabla ya kuondolewa kupelekewa katika chumba cha kuhifadhia maiti

Mvulana huyo ambaye bado hajajulikana wazi ni nani ni miongoni mwa kundi la wanafunzi 106 kutoka shule ya upili ya Molapo.

Maafisa wanachunguza kisa hicho kwa makini.

Wanafunzi wenzake na walimu wanaosemekana kufadhaishwa mno, wanapokea ushauri.

Mlinzi mmoja aliyekuwa katika eneo hilo ambaye ameomba asitajwe, alikuwa ameketi nje ya duka linalouza magari karibu na eneo hilo.

" Basi liligonga bango hili kwanza, kila mtu alikuwa ndani... Kisha mvulana alitoa kichwa nje ya dirisha alikuwa ameketi karibu na nyuma- alijaribu kuona kilichokuwa kinafanyika, na muda sio muda, aligongwa na bango hilo," ameliambia gazeti la Durban Mercury.

"Kila mtu alikuwa analia, walimu, wanafunzi; kulikuwa na kizaazaa. Nilitaka kusaidia lakini sikuweza. Bado alikuwa anapumua - damu zilimvuja - nilipomfikia. Lakini sikuweza kumfanyia chochote," alisema shahidi mwingine.