Watahiniwa wapewa masharti ya mavazi India

Image caption Wanafunzi

Mamlaka nchini India imetoa masharti kwa wanafunzi wanaokalia tena mtihani wa shule moja ya kusomea matibabu.

Mwezi uliopita ,mahakama ya juu iliwaagiza zaidi ya wanafunzi laki sita kurejelea mtihani huo baada ya kubaini kwamba mtihani huo ulikuwa umeibiwa.

Wanafunzi wanaokalia mtihani wametakiwa kuvaa nguo nyepesi zilizo na ukosi mfupi pamoja na mashati yasio na vifungo vikubwa.

Hawawezi kuvaa vipuli wala kubeba kikokotozi ama calculator.Viatu vya kuziba havitakikani isipokuwa vile vilivyo wazi.

Image caption inayovaliwa na watahiniwa nchini India

Nchini India wanafunzi wanaodanganya katika mtihani hukamatwa wakiwa wameficha vifaa vinavyotumia blue tooth na kadi za simu zilizoshonwa katika mashati yao.

Katika kipindi cha miaka michache iliopita,wanafunzi kadhaa pia wamepatikana wakitumia vipaza sauti vya masikioni na kamera zinazowekwa katika vifungo.

Kalamu zinazotumia blue tooth pia hutumika.

Msharti hayo ya nguo yanalenga kuzuia maeneo yanayoweza kuficxha vifaa hivyo.