Watalii wa Uingereza kuondoka Tunisia

Haki miliki ya picha getty
Image caption Tunisia

Maelfu ya watalii wanajiandaa kuondoka nchini Tunisia kufuatia onyo kutoka kwa serikali ya Uingereza kwamba huenda kukatokea shambulio jingine la kigaidi.

Muungano wa mawakala wa shughuli za uchukuzi nchini Uingereza umesema kuwa wanachama wake wanalenga kuwarudisha nyumbani wateja wao katika kkipindi cha saa 48 kinachokuja.

Watalii 38 wengi wao wakiwa raia wa Uingereza waliuawa na mshambuliaji katika hoteli moja nchini humo mwezi uliopita.

Image caption Tunisia

Uingereza imesema kuwa usalama zaidi uliowekwa tangu tukio hilo hautoshi.

Balozi wa Tunisia nchini Uingereza Nabil Ammar ameishtumu Uingereza kwa kuitikia wito wa magaidi.

Image caption Mshambuliaji wa Tunisia

Kati ya watalii 2500 na 3000 wa Uingereza wanaaminika kuwa nchini Tunisia pamoja na wasafiri huru 300.