Walioteketeza kanisa Israeli wakamatwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Walioteketeza kanisa Israeli wakamatwa

Polisi wa Israil, wamewakamata watu kadha, wanaoshukiwa kuchoma moto kanisa mwezi uliopita, katika bahari ya Galilaya.

Wakristo wanaamini kuwa hapo ndipo Yesu Kristo aliwakirimu maelfu ya watu, akiwa na mikate na samaki wachache.

Maandishi iliyolalamika juu ya "kuabudu miungu ya uongo" ilipatikana kwenye ukuta baada ya shambulizi hilo.

Maandishi yalikuwa katika lugha ya Kiyahudi.

Kwa mujibu wa maafisa wa upelelezi hiyo ilikuwa ishara ya kuwa waliochoma moto kanisa hilo walikuwa Wayahudi wenye msimamo mkali.