Waziri mkuu wa Serbia Vucic apigwa mawe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri mkuu wa Serbia Vucic apigwa mawe

Waziri mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic,amepigwa mawe na kufukuzwa na raia wa Bosnia katika hafla ya ukumbusho wa miaka 20 ya mauaji ya halaiki ya watu katika mji wa Srebrenica

Waziri huyo alilazimika kutorokea maisha yake bada ya kutupiwa chupa mawe na matusi.

Mashamblizi hayo yalitokea bwana Vucic alipokuwa akiondoka kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika makaburi ya takriban wahanga 136 wa mauaji hayo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Inaaminika kuwa waziri Vucic aligongwa na jiwe kichwani.

Inaaminika kuwa waziri Vucic aligongwa na jiwe kichwani.

Vikosi vya majeshi ya Bosnia Serb viliwaua wanaume 8000 waisilamu na wavulana wa Srebrenica baada ya kuvamia kambi ambayo ilistahili kulindwa na umoja wa mataifa.

Mauaji hayo yanadaiwa kuwa ndiyo yaliyoisababisha Yugoslavia kuvunjika.

Image caption Hii leo sherehe hizo zitakamilika kwa maziko ya waathiriwa136

Hii leo sherehe hizo zitakamilika kwa maziko ya waathiriwa136 ambao mabaki yao yalitambuliwa hivi majuzi kwa kutumia DNA.

Rais wa zamani wa marekani Bill Clinton ni mmoja wa wale wanaodhuruia maadhimisho hayo.

Awali waziri mkuu Vucic alikuwa ametoa risala za rambirambi japo aliepuka kukiri kuwa yalikuwa mauaji ya halaiki.