UN yakashifu kufurushwa kwa Uighur Thailand

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption UN yakashifu kufurushwa kwa Uighur Thailand

Shirika la habari la taifa la Uchina, xinhua , linadai kuwa watu zaidi ya mia moja wa kabila la Uighur, ambao hivi karibuni waliondoshwa Thailand kwa nguvu walikuwa wakielekea Mashariki ya Kati, kuwa wapiganaji wa makundi ya kiislamu.

Video iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa, inaonesha watu wa tabaka la wa-Uighurs wakiwa wamefunikwa nyuso zao na kuzungukwa na polisi wakirudishwa Uchina kwa ndege.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wa jamii hiyo walionekana wamefunikwa nyuso zao

Kuondoshwa kwao Thailand siku ya alhamisi, kulichochea malalamiko makali kutoka Umoja wa Mataifa, Marekani, na mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu, ambayo yanafikri huenda watu hao wakaadhibiwa na serikali ya Uchina

Kuna wanaofikiri kuwa hao wa-Uighurs walikuwa tu wanakimbia mateso ya Wachina, katika eneo la kabila hilo, Xinjiang.