Mkutano wa dharula waendelea Ugiriki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Viongozi wa Ukanda wa euro wakijadiliana jambo huko Ugiriki

Viongozi wa umoja wa ulaya bado wamejifungia kwenye mazungumzo ndani ya mkutano wa dharura wakijaribu kupata mapatano ambayo yanaweza kuiwezesha Ugiriki kuepuka kuishiwa fedha na kubaki kwenye sarafu moja.

Waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras, anatamani kufikiwa kwa mapatano kwenye mazungumzo hayo kabla benki za ugiriki kuanguka , matarajio ambayo yanaweza kuwa siku chache tu karibuni. Rais wa Benki Kuu ya Ulaya, Mario Draghi, amesema ameshindwa kuidhinisha fedha zozote bila ya mpango wa dharura wa kuokoa uchumi. Wakopeshaji wa Kimataifa wana kadiria kuwa Ugiriki inaweza kuhitaji hadi euro bilioni themanini na sita ili kuepuka kuanguka kiuchumi.

Mawaziri wa ukanda wa sarafu ya euro wameripotiwa kuanda mipango madhubuti ya mageuzi ambayo yataitaka bunge la Ugiriki kupitisha iwe sheria na wachunguzi wa fedha kutumwa Ugiriki. Mwandishi wa BBC huko Athens anasema Tsipras anaweza kuwapanga upya mawaziri wake wiki hii.