Mazungumzo Nyuklia Iran yaleta matumaini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi ya viongozi katika mazungumzo ya Nyuklia ya Iran.

Ikulu ya Marekani imesema kuwa mazungumzo ya Viena kuhusu makubaliano ya Nyuklia ya Iran,ymaefikia katika hatua nzuri.Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kuna mambo ambayo hayajapatiwa ufumbuzi.

Mataifa sita yenye nguvu duniani,ikiwemo Marekani ,Urusi na Uingereza yamekuwa yakifanya mazungumzo na Irani kwa siku 17 sasa kuitaka nchi hiyo kupunguza harakati zake za Nyuklia ili iweze kuondolewa baadhi ya vikwazo vya kiuchumi.

Muda wa mwisho uliwekwa kufikia makubaliano hayo hadi sasa umekwisha.