Hisia kutoka Marekani na Iran

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Obama amesifu mapatano hayo

Rais wa Marekani Barrack Obama amesifu makubaliano baina ya Mataifa sita makubwa yenye nguvu duniani na Iran kuhusiana na mradi wake wa kinyuklia.

Rais Obama amesema kuwa hii ndiyo nafasi ya pekee na ya hakika itakayoizuia Iran isitengeze silaha za kinyuklia.

Obama ameonya kuwa atazima jaribio lolote la bunge la Congress la Marekani kupinga kupitisha makubaliano hayo kuwa sheria.

''Nataka kutoa onyo kwa bunge la Congress la Marekani, Nitatumia kura ya turufu kuzima jaribio lolote la kuzima kutekelezwa kwa mapatano hayo ya kihistoria.''alisema Obama.

Haki miliki ya picha ISNA
Image caption Rais Rouhani amesema kuwa amefurahi kuwa hatimaye vikwazo vyote vitaondolewa dhidi ya Iran

Katika hotuba ya moja kwa moja kwenye televisheni, Rais Obama amekaribisha makubaliano hayo akisema kwamba jumuiya ya kimataifa sasa itaweza kuhakikisha kuwa Iran haiwezi kutengeneza silaha hizo za nyuklia.

Amesema vikwazo vitaondolewa taratibu na Iran ni lazima itimize baadhi ya hatua na masharti kabla ya vikwazo vyote kuondolewa.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kulingana na Rais Obama mapatano haya yataizuia Iran kutengeza zana za kinyuklia

Kwa upande wake Rais Rouhani amesema kuwa wamefurahi kuwa hatimaye vikwazo vyote vitaondolewa na fedha za Iran zilizofungiwa ng'ambo zitafunguliwa.

katika hotuba ndefu rais Rouhani amesema kuwa hawakuwa wanaomba washirikika wao kuwaondolea vikwazo bali walishirikiana.

'' hatukutaka kupewa msaada tuliwataka wenzetu tuwasiliane kwa heshma haki na usawa''

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mapatano yataruhusu wachunguzi wa kimataifa kukagua vinu vya kinyuklia vya Iran

''Tulikuwa tunatafuta vitu vinne vikuu katika mawasiliano yetu na washirika wa kimataifa nayo ni

1,utafiti wa kinyuklia uendelee,

2,kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi

3,kuondolewa vipengee tuliyodhania kuwa ni ukiukwaji wa haki zetu katika umoja wa mataifa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wawakilishi wa Iran na mataifa 6 yenye nguvu duniani baada ya kutangazwa mapatano

4, Sera kali za baraza la usalama la umoja wa mataifa dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran kufutiliwa mbali

''Kwetu tumepata kila kitu tulichokuwa tumepangia na hivyo naona kuwa tumefaulu'' alisema rais huyo katika taarifa iliyopeperushwa katika runinga ya taifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ameuambia mkutano huo kwamba majadiliano hayo ya muda mrefu yamaefanikisha kukabiliana na vikwazo vyote vigumu vya miaka kumi iliyopita.

Amesisitiza kwamba Iran haijakuwa ikijaribu kuunda silaha za nyuklia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapatano yakitangazwa

Bwana Zarif amesema yaliyomo kwenye makubaliano hayo ni magumu mno, lakini hayakuwa makubaliano tu bali ni njia ya kuelekea kutatua uhasama wa muongo uliopita.

Vikwazo vya kiuchumi ikiwemo mabilioni ya fedha mali ya Iran iliyokuwa imefungiwa katika mabenki ya nje ya nchi inatarajiwa kuachiliwa katika siku za hivi karibuni.

Vikwazo hivyo vilivyozuia Iran kuuza mafuta na gesi yake katika soko la kimatifa vilevile ilizuia usafiri wa ndege na meli taifa hilo kuingiza bidhaa ambazo sio muhimu.

Awali Katika mkutano wa waandishi habari huko Vienna mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini alisema makubaliano hayo yanadhihirisha uwajibikaji wa pamoja kwa amani na kuifanya dunia kuwa salama.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Israeli ameonya kuwa mapatano hayo ni makosa makubwa

Bi Mogherini Alisema mapatano hayo yamechangia kufikia masharti na malengo ya jamii ya kimataifa ya kuunda uhusiano.

Rais wa Iran kwa upande wake amesema kuwa ''mapatano hayo yamezuia taharuki ilikuwa bila sababu dhabiti''