Mpaka:Kenya itajitetea dhidi ya Somalia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mpaka:Kenya itajitetea dhidi ya Somalia katika mahakama ya kimataifa

Serikali ya Kenya imesema kuwa iko tayari kukabiliana na Somalia katika mahakama ya kimataifa ya haki (ICJ) kutatua mzozo wa mpaka baina yao.

Mkuu wa sheria wa Kenya, Profesa Githu Muigai ameiambia BBC kwamba Somalia haina haki kudai umiliki wa bahari ya Kenya.

Amethibitisha kwamba kumekuwa na mashauriano ya kutoa kandarasi kwa makampuni ya kimataifa kutafuta mafuta na gesi katika eneo hilo.

Serikali ya Somalia leo inatarajiwa kuwasilisha kesi katika mahakama hiyo ya ICJ baada ya kudai kwamba nchi hizo mbili haziwezi kutatua suala hilo nje ya mahakama.

Somalia inaidai kuwa Kenya inamiliki sehemu ya bahari kwa njia isiyo halali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud

Mgogoro huu umekuwa ukiendelea kwa miaka sita sasa.

Somalia inadai kuwa Kenya imekataa kusuluhisha mzozo huo nje ya mahakama.

Somalia na Kenya zinazozania sehemu ya bahari kusini mwa Kenya eneo linadaiwa kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta na gesi .