Waliovalia sketi fupi waachiliwa huru Morocco

Haki miliki ya picha Yastock
Image caption Waliovalia sketi fupi waachiliwa huru Morocco

Mahakama moja huko Morocco imewaondolea lawama wanawake wawili waliokuwa wameshtakiwa kwa kuvaa mavazi yasio kuwa na heshima mbele ya umma.

Kesi hiyo ilizusha shutuma nchini humo mbali na maandamano yaliyowapeleka wanawake mabarabarani.

Wakili wao ametaja uamuzi huo kama ushindi kwa wateja wake pamoja na wanachama wa chama cha kiraia waliowafanyia kampeni ya kuachiliwa huru.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Kesi hiyo ilizusha shutuma nchini humo mbali na maandamano yaliyowapeleka wanawake mabarabarani.

Wanawake hao ambao ni wasusi walio na umri wa kati ya miaka 23 na 29 walikamatwa mwezi uliopita wakiwa wamevaa sketi fupi walipokuwa sokoni katika mtaa wa Agadir, wakielekea kazini.

Sheria ya nchi hiyo inasema mtu akipatikana na hati ya kuvaa mavazi yasio na heshima huenda akafungwa kifungo cha hadi miaka miwili gerezani.