Mgogoro wa mpaka Kenya na Somalia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud

Serikali ya Somalia leo hii itafungua rasmi kesi dhidi ya kenya katika Mahakama ya kimataifa (ICJ) kufuatia mgogoro wa mpaka baina ya nchi hizo mbili.

Mwandishi wa BBC wa Idhaa ya Kisomali Mahammud Ali anasema Somalia inailamu kenya kuwa inamiliki sehemu ya bahari kwa njia isiyo halali.

Mgogoro huu umekuwa ukiendelea kwa miaka sita sasa.

Somalia inaipeleka Kenya katika mahakama ya kimataifa huko The Hague Uholanzi kwa madai kwamba kenya imekataa usuluhishi nje ya mahakama.

Somalia na Kenya zinagombea sehemu ya bahari kwa madai kuna mafuta na gesi katika eneo hilo.