Dawa za kulevya zaleta vurugu Mexco

Haki miliki ya picha AP
Image caption Joaquin Guzman mtuhumiwa nguli wa dawa za kulevya duniani.

Waziri wa mambo ya ndani wa Mexco ameitisha mkutano wa magavana wa majimbo ili kujadili namna ya kuepusha vurugu zinazoweza kutokea kufuatia kutoroka kwa mtuhumiwa maarufu wa biashara ya dawa za kulevya.

Vyombo vya usalama ndani ya Mexico na maeneo ya jirani kwa sasa vina msaka Joaquin Guzman anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara nguli wa dawa za kulevya anadaiwa kutoroka katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni ya rushwa.

Naye Rais wa Mexco, Enrique Pena Nieto, anasema kuwa ana Imani kuwa idara za usalama zinamkamata mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa mhimili duniani kwa biashara hiyo ya dawa za kulevya na ambaye alitoroka kutoka kati kati ya ulinzi mkali.

Hata hivyo Rais Pena Nieto amesisitiza kuwa uchunguzi wa kina unatakiwa ili kumbaini aliko Joaquin Guzman.