Sketi fupi zawaponza wanawake Morocco

Haki miliki ya picha

Wanawake wawili raia wa Morocco waliofikishwa mahakama baada ya kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu, kwa kosa la kuvaa sketi fupi,hatimaye wameachiliwa huru.

Wanawake hao wawili walikamatwa mapema mwezi uliopita katika maeneo ya soko la Inezgane karibu na Agadir,baada ya kuzuiliwa na wafanya biashara wa soko hilo.

Kesi ya wanawake hao ilikuwa na mvuto wa kipekee katika nchi nzima ya Morocco na hata katika mitandao ya kijamii nchini humo ,na pia kulikuwa na harakati za kutaka kusainiwe hati ya kutaka kutenguliwa kukamtwa na kushambuliwa kwa wanawake hao na kuita jaribio hilo kama kuingilia uhuru binafsi ;ikawavutia maelfu ya watu waliotia saini hati hiyo.

Na kufuatia mvuto wa kesi hiyo na hali ya kuitishwa kwa hati hiyo kuliwavutia wanasheria kadhaa nchini humo,ambao walikuwa tayari kuwatetea wanawake hao kwa gharama zao.

mwanaharakati wa haki za wanawake na mwendesha kampeni dhidi ya jinsi hiyo, Fouzia Assouli ameliambia shirika la habari nchini Ufaransa AFP kwamba kuachiliwa kwa wanawake hao kumeonesha kuwa uvaaji wa sketi fupi nchini Morocco siyo kosa la jinai "

Nayo tovuti ya habari nchini humo ya Tel Quel,imemnukuu wakili wa wanawake hao , Houcine Bekkar Sbai,akisema kwamba baada ya kuachiliwa kwa wanawake hao,kinachofuata ni kuwafikisha mahakamani watu waliowafedhehesha wanawake hao sokoni.