Matembezi ya kuweka amani yaanza Kenya

Image caption Wanariadha wa kenya wafanya matembezi ya siku 22 kuhamasisha amani

Wanaridha nchini Kenya wakiwemo wale waliovunja rekodi za dunia wameanza matembezi ya amani ya siku 22.

Metembezi hayo yatakayochukua umbali wa kilomita 800 dhidi ya ghasia za kikabila yameandaliwa na aliyekuwa mshindi wa mbio za marathon za mashindano ya nchi za madola John Kelai.

Wajomba zake watatu waliuawa katika uvamizi wa mifugo.

Matembezi hayo yalianza kaskazini mwa Turkana na yataelekea kusini kupitia maeneo yenye utata.

Wanariadha hao watabeba tochi kama ile ya mashindano ya olimpiki .

Mwanariadha wa Ethiopia Haile Gebrselassie amesema kuwa atashiriki mwisho wa matembezi hayo.